Tuesday, May 15, 2012

TAFSIRI YA KUWA SINGO BONGO NI MAUZAUZA

Hivi maana halisi ya kuwa Single ni nini??Kuna watu wako Single kweli??Na how long mtu unaweza kuwa Single na ukawa happy tu bila kuwa na stress ukiona wenzio wanasafiri kwenye MV Mapenzi wakati wewe Jahazi lako limezama Nungwi kitambo..

Nna mashaka na watu wanavyotafsiri neno Single...Unakuta mtu kakazana ooh Am a divaaaa,am single and very happy,unapishana nae kwa bahati mbaya Machimachi Guest h...ouse anatoka na jamaa,huyu yuko Single au Plural??au yule jamaa anatumika kama AC tu kupuliza wakati wa Joto?Hapa sielewi..

Mimi nnavyojua single ni mtu ambaye hana uhusiano wowote na jinsia nyingine,wala hachakachui kwa kujificha,sasa hapa Tanzania naona single ni kutokuwa na uhusiano wa kueleweka huku unachakachua kwa kujifichaficha,ukiulizwa ooh mi single...

Single sio mchezo,Hormone zinatengenezwa mwilini kila siku,mwili unapata moto kama pasi ya mkaa kila siku halafu upo tu,eti single,singo kumbatia mito mwaka mzima...Chezea usingo wewe..wangapi mko singo hapa???SIDHANI

No comments:

Post a Comment