Tuesday, May 15, 2012

JIFUNZE KUGUSA MOYO WA MTU...ATAFEEL SPECIAL,UKIGUSA KIFUA TU THERE WILL BE NO CHANGES

Kuna nyakati unapata mtu,mpenzi wa ukweli sana,anabadilisha maisha yako,anakupa raha zote za dunia,zaidi ya yote anaugusa moyo wako in a special way,hadi unajisikia vibaya akiwa hana raha,akilalamika unaona naam kweli huyu anastahili kulalamika maana amekugusa moyo kwelikweli.....

.Ila wakati mwingine,unakumbana na vifurugobe,maneno mengi matendo sifuri,kutwa kucha kulalamika ooh hunijali,hunipendi... vile mimi nataka.kabla hujamlalamikia mtu kwanini hakupendi,jiulize Je,umemgusa Moyo wake pale kwenye Garden Love ya moyo??wengine mnagusa Kifuani tu mnataka mpendwe,kugusa Moyo wa mtu sio mchezo,kumfanya ajisikie yeye ni part ya Moyo wako,akiumiza moyo wako ni sawa na kujiumiza yeye mwenyewe..inataka muda,inataka commitment,inataka uelewa...

Unagusa kifua tu unalalamika,waliogusa Moyo watafanyeje??Cha ajabu,wanaogusaga moyo wako wachache,na ukimpata huwa hadumu sijui kwanini yarabi toba,mtihani kweli,wagusa Vifua wako teleeee,hata hapo wapo...Hamjambo Chest Touchers???Learn to touch the heart,lasivyo Mapenzi yatawapiga chenga deile kama Messi anavyosumbua mabeki

No comments:

Post a Comment