Tuesday, May 15, 2012

UHUSIANO BORA HUJENGWA NA WEWE MWENYEWE,VILE UNAVYOISHI KWENYE UHUSIANO HUO

Ukitaka uwe na uhusiano wenye afya (Healthy Relationship),na uweze kufikia ndoa yenye furaha na amani na ya muda mrefu,na sio hizi harusi za kiduku hazivuki hata Probation miezi 6 inabidi uwe mtu wa kawaida na uwe disminder wa vitu vidogo,usiwe too excited na maisha ya ndoa,ndoa sio Mbinguni,ni duniani hapahapa sema unapunguziwa dhambi kidoogo kuikwepa ile dhambi ngumu ya amri ya 7-1,si mnaijua?

Ukijifanya wewe askari wa Uhamiaji,unafuatilia kila kitu cha mpenzi wako,unapekuapekua simu,mara password,mara nitajie listi ya ex wako,mara kwann huyu ex wako bado anaongea na wewe,mara kwanini FB hauniweki in a relationship with me, utajikuta unazeeka na Moyo wako utaota yale Matege ya Kichaga...

No comments:

Post a Comment