Tuesday, May 15, 2012

UONGO WA FACEBOOK...TEXAS KUMBE ANAKAA KWA MTOGOLE

Hivi kwani kuishi Tanzania kuna kosa gani?Kuishi nje ya Tanzania kunaongeza nini??Uzuri?ama ukiwa nje ya Tanzania kama ulikuwa na matege yananyooka ukiwa huko nini?Kuna watu wameandika wako Manhattan,mwingine Beverly Hills,mwingine yuko Massachussets sijui,wakati jana tu nimemuona anaagiza Chips hapa Corner Bar

Kwani ukisema unaishi kiwalani bom Bom unageuka rangi unakuwa mweusi na Ukisema uko California unaongezeka kuwa na Miguu mi3?
Watu wengine feki kwelikweli...California ya Sinza kwa Remmy?

Facebook kazi kwelikweli..haya mie naishi Mwenge,sijui ndo Boston..dah,kweli ndo maana wachina wamesambaa,maana watu wame-opt kuwa feki hadi roho zao

No comments:

Post a Comment