Tuesday, May 15, 2012

WANAWAKE WA SIKU HIZI NA MIZINGA KWENYE UHUSIANO,WIKI TU TAYARI USHAPIGWA MWIBA

Kama Wanawake wataendelea na hii tabia,sitoshangaa wanaume kuendelea kuweka mgomo wa kuoa na kuendelea kulalamikiwa kwamba wanawachezea...

Hivi inakuwaje unaanza uhusiano na mtu,hata wiki hujamaliza unaanza kumwambia Baby naomba kama una laki 3 haina kazi ya haraka haraka natakiwa nikakomboe dressing table yangu kwa fundi...Laki 3 ya haraka haraka??Mshahara wenyewe tu sipewi haraka haraka nausubir...i hadi mwisho wa mwezi,we hiyo haraka haraka itatokea wapi??Kama unadhani kuna hela ya haraka haraka itafute uone,mbona we hauna?Dressing Table uweke oda ww,mimi sikuwepo,halafu kuilipia unapiga mzinga huku...haya hilo moja.

..Mara utasikia Baby naomba hela nipande Bajaj daladala ntachafuka,sio mbaya its ok,sh ngapi Bajaj itakutosha..Elfu 30..khaaKwani siku hizi kuna Bajaj za Dar kwenda Moro?Arrgh bora chama la Bachela,wizi mtupu...Bado hujaombwa hela ya BBM ime-expire.Si ununue mwenyewe,kama huna na wewe Expire...

No comments:

Post a Comment