Sunday, June 3, 2012

HATA MUUZA JENEZA HUSALI APATE WATEJA NA KUJIBIWA MAOMBI YAKE

Kitu kimoja kuhusu Mungu,hana upendeleo hata kidogo..Unaweza kudhani kuna watu flani anawapendelea na kuwaonea baadhi,lakini kamwe hayuko hivyo!

Fikiria,Jambazi kabla halijaenda kuiba linawaza,na kumuomba Mungu liibe salama lisikamatwe,na linafanikiwa,Mungu hajalala,ameona kila kitu...Wewe unalalamika kuibiwa mwenzio ameshapata mkate wa kila siku...Ingawa hukumu yake Mungu anayo mkononi

Lakini umewahi kuwaza hili??

Una mgonjwa hospitali yuko mahututi,mtu wa muhimu sana maishani mwako,,,Ni mke/mme,unampenda kweli...Au pengine ni mzazi wako,Mama au Baba,unaomba na kusali sana kwamba apone na kurejea...

By the time wewe unasali na kuomba apone,Kuna mtu yuko huko mtaani,ana wiki nzima hajauza Jeneza hata moja...Ana mke na watoto wa kulipa ada...Anafunga na kusali sana Mungu amuangazie baraka kwenye biashara yake...

Kipenzi chako,uliyemuombea sana...Anakufa.....Unakwenda kwa Muuza Jeneza kununua ili umzike...Kwake yeye ni zaidi ya Biashara...Mungu amejibu Maombi yake...Amepata hela,ya kula,na kulipa Ada ya watoto..au hata kulipa kodi with expense ya kifo cha mpenzi uliyemuombea...

Huyo ndio Mungu,sio tu Athumani,wala sio Sadiki....

Muuza Jeneza anapiga sala ya Shukrani na anatoa sadaka kanisani kwa kujibiwa maombi yake kwa muda muafaka,wakati wewe uko Msibani unalia kwa Majonzi..

Mwacheni Mungu aitwe Mungu...

No comments:

Post a Comment