Sunday, June 3, 2012

ONDOA VIATU MLANGONI ILI MTU SAHIHI AGONGE MLANGONI

Najua na kuelewa jinsi inavyouma kuona yule unayempenda sana,na unayetamani awe wako,yeye amechukua upande tofauti na uliochukua wewe...Ameamua kumpenda mtu mwingine!

Inauma sana!Na unafeel kama moto kifuani kwako,chuki imekujaa dhidi yake,unatamani ufanye kitu ila huwezi,unakosa raha na unahisi huna bahati maishani..

Pamoja na hilo,pamoja na yote yaliyotokea,USIWE MJINGA! Haitabadilika,the damage is already done,and you cant reverse that,He/She is gone...na ana furaha huko alipo...Anafaidi penzi kule,wewe huku umesinyaa,umedumaa,unakondeana kwa wishes...Unakondeana kama ndama mwenye Kiu...

DO SOMETHING!

Kulia hakutakusaidia...Kususa hali kadhalika,hakutakusaidia...Kuwa Single kutakuumiza tu zaidi..Achilia moyo wako kwa upya,na mtu sahihi atagonga hodi kwenye mlango wa Moyo wako

Ukijifungia kwenye Mafeeling ya mtu ambaye hayupo,aliyesepa na kukuacha Mataa ya Ubungo bila Nauli,pindi akitokea mtu sahihi na kutaka kugonga kwenye Mlango wa Moyo wako,atakuta Viatu kwenye Mlango huo..Ataogopa,atajua ndani kuna mtu kumbe hamna,atakwenda zake.Utaendelea kujihisi huna bahati lakini kumbe ni kosa lako,Umeacha Viatu mlangoni...Viondoe viatu hivyo na Utashangaa Hodi zitakazofuatia Mlangoni

No comments:

Post a Comment