Sunday, June 3, 2012

SI KILA GARI LENYE MSTARI MWEKUNDU NI LINAENDA UBUNGO KIMARA...MENGINE NI MAGARI YA NYAMA

Huu ni ukweli tu,amini usiamini...Unaweza ukaonba basi lina mstari mwekundu ukajua linakwenda Ubungo na Kimara,lakini mengine ni magari ya Nyama,kamwe usilisimamishe utachafuka na michirizi ya Damu..Yamebeba nyama hayabebi abiria!

Sio Kila Gentleman na Smart guy anafaa kukuoa,wengine ni mashoga yamejificha kwenye usmart tu,chunga sana,na yako mengi tu hapa mjini!

Sio kila Mwanamke mzuri atakupa Watoto wazuri,wengine wamechoka wametoa Mimba zaidi ya 23,utaishia kununua vitenge tu na kulegeza chaga kila siku ila watoto Nehi..

Sio kila Cover zuri linasadifu utamu wa kitabu humo ndani,zingine chogi tu ndani utumbo

Sio kila Mpole ana tabia nzuri,usidanganyike,wengine wanajijua wakiongea wanaweza kukupa Heart Attack.

Chunga sana,si kila vionekanavyo hivyo,viko hivyo vionekanavyo,Vingine viko tofauti unahitaji Microscope kuona Inner Particles

No comments:

Post a Comment