Sunday, June 3, 2012

MAPENZI YA JIKO LA KUNI..THATS WHERE WE HAVE ARRIVED

Mapenzi ya siku hizi yako kama Jiko...Tena jiko lenyewe bora lingekuwa la Tambi,angalau ukiweka tu mafuta ya Taa linawaka..

Yamekuwa Mapenzi ya Jiko la Kuni...Ili uwake lazima kuwe na wapuliziaji wengi...Mmoja huku,wawili kule,watatu paleeee...

Wanaume wamekuwa waongo,wanaoa ili watimize wajibu,kwenye Familia zao waonekane wameoa na wako responsible ila kumbe aah wapii! Na wengine wanaoa tu kwa sababu wamekuwa na wapenzi wao kwa muda mrefu,watafanyaje sasa,wanaoa!

Wanawake nao wanaolewa kwa ajili ya Heshima na Title,wanaitwa MRS FLANI....Kama sio hivyo basi wamepata shefa lina hela,hawawezi kuliachia,maisha ya ghorofani wanatema mate kutoka juu

Na wote hawa mafiga 7 kama kawa...Huyu kakamatia mtoto kamuweka ndani akijua katulia kumbe walaaaa,aliyewekwa ndani nae ana mwandani wa Ubani sema ndo kapuku,ila chezo analijua,anajiiba!

Nikiwaza ndoa huwa nahisi mapigo ya Moyo yanapiga kuliko kawaida,Hamna siku nimewaza ndoa nikaishia kusmile,......Ndoa sio matarumbeta na Kwaito....Ndoa ni jukumu,tena la Kimungu sio mchezo,ukiingia jua Mungu yupo kati,Kombolela zote Mwisho..Ila wengi tunachukulia Poa,tunaishi maisha ya HARUSI kwenye NDOA...Harusi inaishia Ukumbini tu,Ndoa ni Balaa,JIPANGENI!

Kila siku zinaibuka Mbinu chafu,Kucheat imekuwa kawaida kama Harufu kwenye Machingio ya Kiembembuzi,hamna anayeshangaa...WAZA UPYA!

1 comment: