Thursday, May 31, 2012

NDOA INAKUPA PETE NA TITLE TU,HAIBADILISHI TABIA YA MTU

Ndoa haibadilishi tabia ya mtu,nyie ambao mna hopes kwamba aah my boy atabadilika tu huko mbeleni tukioana,or my girl atabadilika,habadiliki ng'oo!

 Kama anakupiga ngumi leo be sure atakutandika na mwiko huko ndani...Ukikosea kudhani kwamba Ndoa inakuja na changes utapotea.

Ndoa inakupa pete tu kidoleni na kukuchange title,ila sio tabia.Kama anapenda dagaa leo ndoa haitambadilisha apende matembele.Make the right choices leo lasivyo utakuwa mtumwa wa tabia zake milele.

Kosa kubwa watu hufanya ni kuamini kwa sababu ameamua kuniweka ndani,haya mambo yatakuwa madogo na with time atachange,HAPANA!

Kamwe usithubutu kufanya Assumptions na ndoa,tabia ya mtu kwenye ndoa itaonekana Mapema,huwezi kuona Jua linawaka halafu uwaambie watu sasa hivi ni Sa3 usiku,utakuwa Kichaa.

Ni muhimu kufanya maamuzi sahihi,kwenye muda sahihi,na kwa mtu sahihi,la sivyo,ndoa haitakuwa chaguo sahihi kwako,utajikuta umejifunga kwenye Mateso ya milele!

No comments:

Post a Comment