Thursday, May 31, 2012

UKIPATA MPENZI FRIED CHICKEN MSHUKURU MUNGU SANA,UKIPATA MPENZI MJUSI WA KUKAANGA KAZA ROHO

Kuna aina ya mtu katika maisha,ukimpata akawa mpenzi wako,unasema asante Mungu, umenipa zawadi hii,he/she is a man and a half,ni kama wewe ni Chips umekutana na Fried Chicken with Mayonnaise,ni raha na kila kitu ni utamu tu na kujilamba..

 Ila kuna mtu unakutana nae, anakuwa mpenzi wako,Kiruu!!Ni kasheshe bin vurugu mechi,Hadi unajikuta unakuwa mtaalamu wa kuimba wimbo wa Shaggy, Why me Lord kila s...iku...Ni kama wewe ni Chips halafu umekutana na Mjusi aliyekaangwa na kachumari ya pilipili,sidhani kama utafeel kula labda uwe Mchina mtengeneza barabara.

 Kama umepata mpenzi wa kweli,sali sana,mshukuru Mungu na umuombee,maana ni bahati sana na vita ya kumkeep ni kubwa,sio unachukulia for granted..
 
.Na pole kwa wewe uliyekumbana na Mjusi,fumba macho mmwagie tomato Ketchup,huwezijua anaweza kuwa na ladha ya prawns

No comments:

Post a Comment