Thursday, May 31, 2012

SIO KILA ANAYEBREAK UP NA WEWE HAKUPENDI

NGUMU KUMEZA:

Sio kila anayebreak up na wewe hakupendi,Ni mkatili,Hajali,Ni player,hana shukrani,au amekutumia kama brashi ya Kiwi halafu anakuacha na dawa nyeusi na kukusokomeza chini ya kitanda

Wengine wanaomba Break Up baada ya kujitathmini na kugundua kwamba wewe,ur too good for them na hawastahili hata kidogo kukumiliki,wanaacha mwenye stahili akupate.Sasa wengine wakiachwa wanaanza shombo,Mwanaume atakuwa Yule,Janaume halina shukrani nimelivumilia tangu liko Kapuku hadi leo linajua hata kuweka panga kwenye suruali!

Kama nimegundua una penzi 100% kwangu na mimi nna 20% kwako nifanyeje?80% yote nakunyonya wewe,nakuwa kama kupe,naamua kuwa mkweli kwa nafsi yangu tu,kwanini nikudanganye na kukupotezea muda nije nikudissapoint baadae wakati nimeshajua mapema,naamua kmuachia mwenye 100/100 aje akupe unachostahili

Je,kuna kosa hapo hadi muanze kubweka kama mbwa koko wa mjumbe kisa umetiwa konzi??

No comments:

Post a Comment