Friday, May 11, 2012

UANAUME SIO SURUALI,NI MAJUKUMU

KWENU WANAUME TENA:
Umemdanganya mtoto wa watu unampenda,akakuamini,akasahau hadi tarehe akaona zote ni February 32,umempa mimba mtoto wa watu mzuri tu,amehenyeka na mimba miezi 9 amekuzalia mtoto..ghafla umemtelekeza eti huna plan nae,eti sio chaguo lako,eti mimba ni bahati mbaya tu hukupanga...Uongo mtupu na ghiliba za nyani mzee
Ulivyokuwa unapewa tunda bure,unakatika kwa spidi kama umefungwa i...njini ya boti ya Horsepower 6 ulitegemea nini?Mbona wanaume tunakuwa migumegume hivi lakini?Mtoto wako mwenyewe hata hujui anakula nini,anavaa nini kweli?unatanua na mademu wengine mwanao hujui anaumwa,katibiwaje,kapona au lah kweli?Mngefungwa uterus japo mkae na mimba wiki 3 kama panya mngejifunza kuacha upuuzi huu.LEA DAMU YAKO,we si kidume?.Wanaume wa dizaini hii ni aibu kwa taifa,Ukijifanya Fundi wa kukatika kama Fally Ipupa uwe pia fundi wa kulea!Ukichukia shauri yako ila Uanaume sio suruali,ni majukumu!

No comments:

Post a Comment