Friday, July 13, 2012

USICHUKUE USHAURI WA KIFEDHA KUTOKA WATU WALIOFULIA...DONT TAKE FINANCIAL ADVICE FROM BROKE PEOPLE

Tangu lini Matonya ombaomba atamshauri Manji ajenge ghorofa Samora Avenue??Sanasana atamwambia ghorofa litaanguka blaza bora ufuge ng'ombe hata akiumwa utachinja ule nyama...Narrow thinkers will always give you Narrow Ideas.

 Do not take Financial Advice from Broke people!We unadhani watakushauri nini???Mawazo yao yamefungwa kwenye umaskini,hawaoni opportunities hata zinazopita kwenye Kope za macho... yao,kamwe usiombe ushauri watu hawa,wamefulia kuanzia Mfukoni hadi mawazoni.Ni waoga,na usidhani mtu mwoga atakushauri kitu cha kijasiri.

 Ni sawa na mtu aliyeachika kwenye Ndoa awe ndo Kungwi wako wa kitchen Party,Jiandae kwa talaka tu ndugu yangu!Watu wengi wameshindwa kujikwamua kwenye umaskini kwa sababu tu wameomba ushauri kutoka kwa Wrong people........
Wahenga walisema Ukitaka kunukia waridi kaa na waridi,ukitaka Mafanikio ongea na watu waliofanikiwa,hao wanazo mbinu za kukufikisha mahali ambako wao wamefika.Division 0 akikufundisha wewe mbinu za kufaulu basi usitegemee utapata Division 1,jiandae kupata Division Negative,kama ipo!
 
Watu wengi wana mawazo yenye thamani ya GOLD,wanaenda kushea mawazo hayo kwa watu wenye thamani ya Madini ya Ulanga....There will be no added Value...Gold should stay with Gold because its more valuable....Labda Ulanga uje kwa Gold ili uongezewe thamani,and not vice versa.
 
Your finacial Breakthrough itategemea na aina ya watu unaowakaribisha katika maisha yako,hawa wana-kuaffect kwa namna moja au nyingine...Kama wewe hutawaaffect wao,basi watakuaffect tu....Wataua ndoto zako kubwa kwa sababu wao hawana ndoto kabisa au ndoto zao ni za kitoto.
 
Amua leo,Je,una ndoto kubwa ya ku-achieve???Look for the right people to nourish it....Sit down with them,watakuonyesha njia
 
Ukiendelea kukaa na hao wasio na msaada utabakia hapohapo na usipoangalia utaanguka kabisa.
 
UAMUZI NI WAKO!

2 comments:

  1. oohh kumbe .. ila maskini anatakiwa anishauri nini sasa..jinsi ya kulia au jinsi ya ku savaivu kone njaa

    ReplyDelete
  2. Kila mtu ana wazo la ziada nakubaliana nawe lakini pia ni vyema kuheshimu na kuthamini mawazo ya kila mtu ndio maana kura moja ya masikini ina thamani sawasawa na kura moja ya tajiri

    ReplyDelete