Wednesday, May 16, 2012

DONT TRUST NOBODY,MASHOSTI WAMESHAKUWA FEKI NA WASALITI

Hii ni kwa wale wadada ambao wao ukikosea njia tu ukawatambulisha Boyfriend au Mchumba wako kwao,basi andaa Sanda ya Mazishi yako mwenyewe..Wako fasta kuliko Bluetooth ya Simu ya kichina...

Watamtega na vinguo,watajifanya Shem umepeneza,Shem I miss you,Shem siku hizi huonekani...Mara Shem kuna mMende chumbani kwangu naogopa kulala...Mwishowe Mende anakuwa Mende,maana Mene akifa analala Chali..

Hawa wanaitwa She Doesnt Mind Generation...Hata Sean Paul amewaimba kwenye Album yake ya Tomahawk Technique...Mkome kabisa hii tabia,Shosti kakuamini,tena siku hizi wanaitana BFF...Utashangaa jinsi BFF anavyopindua Nchi yako bila kutumia Jeshi wala Manowari

Mtakuja kuchomwa pasi sehemu za 'kinyume cha wazi',Acheni hii tabia sio nzuri

No comments:

Post a Comment