Tuesday, May 15, 2012

KAMA UMEMCHOKA NA HUMPENDI MWAMBIE,KUKAA NA MAITI NDANI SIKU NYINGI HAIMAANISHI ATAFUFUKA

Huwezi kumshawishi Nyani Mzee kwamba Asali ya Nyuki ni tamu kuliko Ndizi zilizoiva

,Huwezi kumfanya Twiga aamini kwamba Ng'ombe anafaidi zaidi kula majani kuliko yeye anavyofaidi kula matawi ya Miti...
Penzi lililokufa halitibiki kwa Dichlofenac wala Ramli ya Dk Manyaunyau,likifa limekufa...Ukihisi humpendi tena usipoteze muda kuremba wala kuona aibu wala hata kuogopa ataumia,ni sawa na kutembelea ...tairi yenye pancha unaumiza tu ringi,toa tairi funga mpya,u cant escape the cost..

.Mwambie tu ukweli,atalia,ataenda kwa Mangi atanunua leso,atapona atasonga mbele,ni afadhali aumie sasa hivi apone kuliko kumuweka pending aje kuumia baadae,maumivu ni maumivu tu,hayana exchange rate kwamba unasave dola,

 if Love is dead its dead...kukaa na maiti ndani haimaanishi atafufuka ni bora umtoe nje akazikwe usubiri Arobaini

No comments:

Post a Comment