Tuesday, May 15, 2012

UKIPENDWA NA MTU MSHIKILIE KWA MIKONO MITATU,UKIACHIKA UTALIA,MTAANI HAKUFAI

Ukigundua unapendwa Shikilia hapohapo,tena kwa mikono mitatu,kama unayo,ukijifanya watafuta na wewe eti upate feling ya kupenda utaangukia usipopendwa..

Wanaume na wanawake wa Tanzania hii wameshasahau kupenda ni nini,wameshatendwa nje na ndani,mioyo yao imetoboka ina matundu kama Chandarua,inavuja kila upande,wewe una-invest Love kwenye Moyo wake inatoka saa hiyohiyo kama bomba la Dawasco lililopasuka..

Ukimpoteza huyo anayekupenda utasota kupata penzi la kweli hadi moyo wako utakuwa kama kisigino cha Mmachinga kwa msako wa True Love.,utakumbana na Vyandarua tupu huku nje utashonea kila kiraka na penzi litavuja kama kawa..

.Shikilia uliyenaye ohooo,we ning'inia kama antenna ya tubelight,akiachia huyo utasimulia hadi wajukuu...

No comments:

Post a Comment